Martin Ahadiel Animal Health Care

Martin Ahadiel Animal Health Care Tunatoa ushauri,matibabu na huduma mbalimbali za mifugo kwa wafugaji wote popote ulipo.Tunapatikana Morogoro. .

Karibu tuzungumze juu ya ufugaji bora na wa kisasa wenye TIJA na MANUFAA. . Tuwasiliane kupitia
MartinAhadiel Animal Health Care
0

24/01/2021

Parvovirus Infection (Kwa kifupi uitwa Parvo)
Ugonjwa huu ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi ambapo mara nyingi hushambulia mbwa wadogo wenye umri wa kuanzia wiki sita mpaka miezi sita. Ugonjwa huu ni moja ya ugonjwa mbaya sana kwa mbwa kwasababu unapomuingia tu basi matumaini ya kupona kwa mbwa huyo ni madogo sana kwasababu ni ugonjwa ambao ukimpata mbwa ndani ya masaa 24 unaweza kupelekea kifo kwa mbwa huyo.
Ugonjwa huu husambulia sana mapigo ya moyo na kupelekea mapigo ya moyo ya mbwa huyo kwenda mbio sana, na kumfanya hapoteze hamu ya kula, joto kushuka sana.
Hizi ndio dalili kubwa sana za ugonjwa huu wa Parvo ni Kuharisha damu, Kutapika, kukosa hamu ya kula, kupungua uzito ghafla. Mara umuonapo mbwa wako ana dalili hizi basi unashauriwa kuwasiliana na mtaalamu wako wa wanyama kwaajili ya ushauri na matibabu zaidi ijapokuwa k**a mbwa huyo hakuwahi kupatiwa chanjo ya Ugonjwa huo tokea utotoni basi asilimia ya kupona ni ndogo sana kwa maana unapoona dalili za ugonjwa huu basi ni dhahiri unakuwa ushamshambulia sana mbwa huyo.

Nini husababisha ugonjwa huu wa Parvo?
Mara nyingi ugonjwa huu usababishwa na mbwa aliyehathirika moja kwa moja na ugonjwa huu japokuwa kuna sababu nyingine k**a endapo mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu anapojisaidia haja kubwa na mbwa mwingine akapita kunusa basi mbwa huyo anakuwa anaambukizwa moja kwa moja. Inasemekana virus vya ugonjwa huu vinauwezo wa kuishi kwenye udongo kwa takribani mwaka mmoja na ugonjwa huu unaweza kuambukizwa moja kwa moja kutoka kwa mbwa mmoja kwenda kwa mbwa mwingine.

Vilevile Ugonjwa huu unaweza kuletwa na viatu endapo mtu amekanyanga kinyesi cha mbwa aliyeathirika na ugonjwa huu basi anapoingia nyumbani au kwenye mazingira ya mbwa ni rahisi sana kuacha virusi hivyo na ikumbukwe kuwa virusi hivi huishi kwa takribani mwaka mzima kwenye udongo.

Unapohisi umekanyaga kinyesi au kitu chochote ambacho kinaweza kuwa na virusi vya parvo basi unashauriwa kusafisha eneo hilo kwa kutumia madawa ya kuua virusi kwaajili ya kujirinda na ugonjwa huo hatari.
Tiba ni Ipi kwa Ugonjwa Huu?

Inavyosemekana mpaka sasa hakuna tiba sahihi ya ugonjwa huu

     >Huu ni ugonjwa ambao mtu/mnyama huupata pale anapong'atwa na mbwa anayeugua ugonjwa huo.>Kichaa hicho cha mbwa ni ...
06/08/2020


>Huu ni ugonjwa ambao mtu/mnyama huupata pale anapong'atwa na mbwa anayeugua ugonjwa huo.
>Kichaa hicho cha mbwa ni ugonjwa ambao asilimia 99 unaenezwa na mbwa baada ya kumng'ata binadamu,kumramba au hata kumkwangua kwa kucha zake.
>Ugonjwa huu huenezwa kwa mate ya anayeugua kugusa jeraha na mnyama aliyeambukizwa.
>Ugonjwa huu huwapata wanyama takribani wote wenye damu moto na hudhibitiwa kwa chanjo pekee.
>Chanjo ya kichaa cha mbwa{Rabies Vaccine} hutolewa kwa mbwa akiwa na umri wa miezi minne na zaidi kisha hurudiwa kila baada ya mwaka mmoja .

NJIA KUU ZA UJUMLA ZA KUDHIBITI MAGONJWA KATIKA KUKUA. Kutunza hali ya usafi ndani ya banda na kudhiditi kusiwe na unyev...
05/11/2019

NJIA KUU ZA UJUMLA ZA KUDHIBITI MAGONJWA KATIKA KUKU

A. Kutunza hali ya usafi ndani ya banda na kudhiditi kusiwe na unyevu
B. Matandazo yakichafuka yabadilishwe.
C. Vyombo vya maji visafishwe kila siku
D. Jitahidi uepuke kufuga kwa njia ya huria ili kuku wako
wasiambukizwe magonjwa kirahisi
E. Epuka kufuga kuku wako pamoja na bata na khanga.Hawa ni
wabebaji wa vimelea vya magonjwa ya kuku japo wao hubaki salama.
F. Zingatia ratiba za chanjo kwa magonja yasiyo na tiba k**a kideri na mengineyo ya virusi

MAMBO YA KUJIEPUSHA NAYO KATIKA UFUGAJI KUKU
Ndugu mfugaji ni ukweli usiopingika wala kujadilika kuwa katika
ufugaji kuna baadhi ya mambo wafugaji tunayafanya lakini hayakupasw kufanyika, yafuatayo ni ya kujiepusha nayo katika ufugaji:-
1. Kuacha banda chafu
2. Kuleta kuingiza kuku wageni bila kujua historia ya chanjo walipotoka.
3. Kuuza kuku wagonjwa.
4. Kuchinja kuku wagonjwa
5. Kununua kuku wagonjwa.
6. Kutupa kuku waliokufa porini.
7. Kununua chanjo kwa wauzaji wanaofahamika kuwa hawana solar power au jenereta.
8. Kutibu kwa mazoea bila kuwasiliana na Afisa Mifugo.
9. Kutembelea mabanda ya jirani bila kuchukua tahadhari.

MAGONJWA YANAYO WAKUMBA SANA MBWAMbwa ni mnyama muhimu sana katika maisha ya binadamu kwani mnyama huyu husaidia katika ...
20/06/2019

MAGONJWA YANAYO WAKUMBA SANA MBWA
Mbwa ni mnyama muhimu sana katika maisha ya binadamu kwani mnyama huyu husaidia katika ulinzi na mapambo katika nyumba, hivyo basi kumtunza mbwa ni jambo la msingi sana ikiwemo udhibiti wa magonjwa na wadudu wasumbufu pamoja na maradhi bora(nyumba/banda), hivyo basi yafahamu magonjwa na wadudu wasumbufu wanaosumbua mbwa kwa sana.
1. KICHAA CHA MBWA (RABIES)
Kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoambukizwa kutoka kwa wanyama hadi binadamu kupitia kwa mate,kwa kung`atwa na mbwa mwenye maambukizi ya virusi vya kichaa. Ambapo mbwa au mnyama aliye patwa na virusi hivi akimng`ata mtu au mnyama mwingine asiye kuwa na kichaa umuambukiza.
Kichaa hupatwa kwa wanyama walio kundi la mamalia,kwa paka wao wanaukinzani kidogo na ugonjwa huu kulinganisha na mbwa.
Mara baada ya kuumwa waweza usione dalili za ugonjwa huu,kwani uchukua muda, kulingana na sehemu uliyo umwa hadi kufikia katika ubongo.
Dalili za awali za kichaa cha mbwa.
(a) Mbwa kujikuna mara kwa mara.
(b) Mbwa kutokwa na mate mengi mdomoni.
(c) Mnyama kupoteza hofu ya kitu chochote.
(d) Mnyama kung`ata vitu ovyo ovyo.
(e) Mnyama kuzunguka ovyo
(f) Mbwa kutependa mwanga na kukaa gizani.
(g) Mbwa kuogopa maji.
(h) Mbwa kuogopa mwanga.
(i) Mbwa kubadili tabia,mbwa mkali kuwa mpole na mpole kuwa mkali ( mbwa huwa na tabia zisizo za kawaida.)
(j) Mbwa kukojoa mara kwa mara.
(k) Mbwa kutopenda vitu halivyovizoea.
Dalili za baadae za kichaa cha mbwa.
(a) Mnyama kupoteza fahamu.
(b) Mnyama kupooza baadhi ya viungo.
KUDHIBITI
(a) Mpatie mbwa wako chanjo kila baada ya muda wa mwaka mmoja.
(b) Kwa mbwa waliokwisha pata kichaa cha mbwa hakikisha wanadhibitiwa vya kutosha, kwani mbwa waliopata kichaa huchukua siku tatu hadi kufa.
(c) Dhibiti mbwa wanaozulula mtaani (zuia mbwa wa mtaani.)
(d) Jina la chanjo ni RABIES .

2. UGONJWA WA MFUMO WA HEWA.
Huu ni ugonjwa unao athiri mfumo wa hewa ikiwemo TB,Phnemonia, ni magonjwa yanayo sambaa kutoka mnyama mmoja kwenda mnyama mwingine kwa njia ya hewa.
Dalili zake,
a) Upumuaji wa shida.
b) Mbwa kushidwa kupumua.
c) Kupumua kwake kunatoa sauti nzito, ule wa kukoroma.
d) Mbwa kukohoa.
e) Mbwa hupumzika mara kwa mara.
f) Mbwa kutoweza kubweka.
g) Kutoka mapovu puani au ute.
Tiba.
h) Mpatie mbwa wako dawa yeyote ya Atibiotic k**a, Otc,penstrep,Tylosin.
i) Pamoja na dawa ya vitamini ambayo itamsaidia kurudisha hamu ya kula.

3. MINYOO (WORMS)
Minyoo ni wadudu wanaosumbua kwa kiasi kikubwa sana katika mbwa hata kwa wanyama wengine wengi wafugwao k**a mbuzi,ng`ombe na kondoo, ambapo huweza sababisha madhara makubwa katika mbwa na kupelekea mbwa kudumaa na hadi kufa.
Dalili za Minyoo katika mbwa ni,
a) Kuharisha.
b) Mbwa kupoteza hamu ya kula.
c) Manyonya kusambaratika.
d) Uzito kushuka.
e) Mbwa kuwa dhaifu.
f) Mbwa kukohoa
Wafuatao ni aina ya minyoo wanao sumbua sana katika mbwa.
1. Minyoo wa mviringo.
2. Minyoo wa kwenye moyo.
3. Minyoo wa kwenye mapafu.
Tiba
Fanya chanjo za minyoo kwa kila baada ya mda wa miezi mitatu, na kwa wale ambapo tayari wamepata ugonjwa wa minyoo wapatiwe dawa ya minyoo ambayo ni IVERMECTIN.

4. UKURUTU (MANGE)
Ugonjwa wa ngozi,na ugonjwa huu uweza kutoka kwa mnyama mmoja kwenda mnyama mwingine,pia hata kutoka kwa mnyama kwenda kwa binadamu.
Dalili.
a) Mbwa kujikuna kupita kiasi.
b) Manyoya kunyonyoka.
c) Gamba gumu ujitengeneza juu ya ngozi.
d) Eneo liliathirika huwa na gamba gumu.
e) Mnyama anakuwa anajikuna mara kwa mara.
Udhibiti.
a) Ogesha mbwa wako mara kwa mara angalau mara tatu kwa kila mwezi,hii itasaidia mbwa kutopata ugonjwa wa ukurutu.
b) Tenga mbwa waliopatwa na ukurutu.
c) Kwa mbwa waliopata tayari ukurutu wapatie dawa ya IVERMECTIN dawa hii imeonesha mafanikio makubwa katika kutibu ukurutu na dawa hii uchomwa katikati ya ngozi na nyama.

5. UGONJWA WA KUTETEMEKA (CANINE DISTEMPER).
Huu ni ugonjwa unaosambaa kutoka mnyama mmoja kwenda mwingine,na ni ugonjwa unapelekea vifo vya mbwa wengi.Ni ugonjwa wenye chanjo zake.
Ugonjwa huu usababishwa na virusi wanaoitwa Canine Distemper Virus(CDV)
Dalili za Ugonjwa.
a) Mgonjwa kutetemeka
b) Mbwa kupooza miguu ya nyuma.
c) Anapunguza kula.
d) Macho yanavimba hadi upofu.
e) Ute ute mwingi kutoka kwenye pua.
f) Kuharisha
g) Dalili ya mwisho mbwa kupooza mwili
Udhibiti.
a) Ugonjwa huu hauna tiba bali ni chanjo inayoitwa DHLP.
b) Chanjo hii apewe mbwa akiwa na umri wa wiki 8 hadi wiki 12.

6. WADUDU WASUMBUFU.
Mbwa akiwa na wadudu hawa hujikuna sana na hujikuna mara kwa mara hasa hasa sehemu za mkia, pia mbwa hukosa raha na muda mwingi hupoteza hadi hamu ya kula kwa usumbufu huu wa wadudu, wadudu hawa sumbufu ni k**a viroboto, kupe, chawa na papasi.
Udhibiti.
- Jinsi ya kudhibiti wadudu hawa ni kuogesha kwa kutumia dawa maalumu Dog shampoo, tik tik na paranex. Kwa dog shampoo imeonyesha kufanya vyema sana kwa kudhibiti na kuua kabisa.
- Usafi wa nyumba wanazo ishi mbwa ni muhimu sana kwa huku ndiko k**a usafi usipo zingatiwa wadudu hawa uzaliana kwa wingi sana, safisha kwa maji safi pamoja na kutumia dawa maalumu ili kudhibiti wadudu hawa, hakikisha dawa unachanganya kwa usahihi bila kudhidisha dawa kwani uweza pelekea mbwa kudhurika.

7. VIRUSI VYA PARVO.
Ugonjwa huu (virusi vya parvo) uwakumba sana watoto wa mbwa wenye umri wa kuanzia wiki 2 hadi wiki 4.Husababishwa na virusi aina ya Canane parvo virus
Dalili,
a) Kuharisha.
b) Kutapika.
c) Wanakosa hamu ya kula.
Tiba
a) DHLP ni chanjo inayotumika kudhibiti ogonjwa huu.
b) Antibiotic k**a OTC hutumika kwa kutuliza tu na sio kutibu magonjwa.

UFUGAJI BORA WA KUKU AINA YA KUROILERKuloirer ni kuku chotara ambaye asili yake ni nchini india, na imetokana na mchanga...
08/04/2019

UFUGAJI BORA WA KUKU AINA YA KUROILER
Kuloirer ni kuku chotara ambaye asili yake ni nchini india, na imetokana na mchanganyiko wa dume la broiler na jike aina ya Rhode island red au dume la white legham na jike la Rhode island red.
Kuku hawa ni moja kati ya kuku wasio na gharama kubwa katika kuwafuga lakini pia wana faida kubwa pindi ukiamua kuwafuga. Lakini pia
kuku hawa ni moja kati ya mbegu ambayo inafanya vizuri sana katika nchi nyingi.
SIFA ZA KUROILER
1. Ni aina ya kuku ambao hutumika kwa matumizi ya nyama pamoja na mayai
2. Kuroiler ni kuku anae fugika katika mifumo yote
3. Pia ni moja kati ya aina ambayo haipati magonjwa kirahisi (disease resistance)
4. Kuku hawa hawana gharama sana katika kuwalisha kwa sababu wanauwezo pia wa kula chakula k**a kuku wa kienyeji.
BANDA
K**a walivyo kuku wengine banda lazima liwe bora ili kuweza kupata kuku bora pamoja na mayai mengi, ila pia kuku wa aina ya kuroiler sio lazima uwafungie ndani moja kwa moja unaweza kutengeneza sehemu ambayo utawafungulia ili kuweza kujipatia chakulatofauti na kuku wa kisasa.
Lakini pia ni vyema kila wakati ukazingatia usafi ni muhimu hivyo ni vyema kuzingatia hilo
CHAKULA
Chakula ni lazima kiwe bora ili kupata kuku bora pamoja na mayai ya kutosha.
1. Muhimu sana kwa mfugaji kujifunza jinsi ya kuchanganya chakula mwenyewe.
2. Kuanzia siku 1 hadi wiki 4 unatakiwa kuwapa chakula cha kuanzia (chick starter mash)
3. Kuanzia wiki ya 4 hadi 8 unawapa chakula cha kukuzia (chick grower mash)
4. Kuanzia wiki ya kwanza kuanza kutaga hadi mwisho unatakiwa kuwapa chakula(layersmash)
5. Katika ufugaji wa kuku hawa ni muhimu kuzingatia lishe bora tangu kifaranga hadi kuanza kutaga, fahamu kwamba matunzo ya kuku anae anandaliwa kwa ajili ya kuja kuwa mtagaji ni tofauti na yule kuku anae fugwa kwa ajili ya nyama. Hivyo kitu moja wapo cha kuzingatia ni lishe bora unaweza nunua dukani au unaweza changanya mwenyewe tu chakula cha kuku wako kwa kutumia formula zuri.

UTAMBUZI WA MWANZO WA MAGONJWA YA MIFUGOSIFA ZA MNYAMA MWENYE AFYA☆Mchangamfu wakati wote macho maang'avu huku mkia masi...
07/04/2019

UTAMBUZI WA MWANZO WA MAGONJWA YA MIFUGO
SIFA ZA MNYAMA MWENYE AFYA
☆Mchangamfu wakati wote macho maang'avu huku mkia masikio vikimsaidia kufukuza inzi
☆Kula na kucheua, kunywa maji vizuri kila siku
☆Kuonyesha ushirikiano wa kutembea pamoja kwenye kundi
☆Kutembea vizuri
☆Anashtuka na kukimbia anaposhtuliwa na mnyama hatari anapomkaribia k**a vike Mbwa mwitu, fisi, chui, simba.
☆Mwili wake una uwezo mkubwa wa kukibadili chakula anachokula kutoa mazao ya kutosha k**a vile maziwa
☆Anaonekana mwenye nguvu na kwa wale wanaoendelea kukua wanaongezeka uzito kwa muda mfupi
☆Kwa mnyama anayekamuliwa mara kwa mara kupiga kelele za kumtafuta mtoto wake, kiwele huwa kimejaa maziwa, chuchu huwa wakati mwingine zimetanuka upande kwa ajili ya kujaa maziwa
☆Ngozi ya mnyama husisimka mara kwa mara wadudu wanapomtambaa
☆Kwa madume, huwa wana hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto. Miili yao hujengeka vizuri. Pumbu hujengeka na kukaa vizuri kwenye nafasi yake (yaani katikati ya miguu)
☆Pua na midomo huwa na unyevu nyevu wakati wote
☆Ngozi huwa na ulaini unaotakiwa na manyoya hung'aa
☆Kwa kawaida unapo mkaribia mnyama endapo amekaa chini ni lazima atanyanyuka
DALILI ZA MNYAMA ANAYEUMWA
☆Hukosa hamu ya kula na kunywa maji
☆Mwili kunyong'onyea na kuonekana mchovu
☆Mnyama kutembea polepole na kwa taabu na mara nyingi hujitenga na wenzake
☆Pua zake na midomo huonekana kupauka
☆Kupunguka kwa kiwango cha uzalishaji k**a vile maziwa. Kwa madume huduwaa na kuinamisha shingo chini na kukosa hamu ya kuwapanda majike wanaoingia kwenye joto.
VYANZO VYA MAGONJWA
☆Magonjwa mengi ya mifugo husambazwa na vijidudu ambao huingia kwenye mfumo wa damu na husababisha homa na baadaye madhara makubwa. Magonjwa mengi ya mifugo husababishwa na vyanzo kutoka nje ya mwili wa mnyama mafano mazingira machafu anayoishi mnyama, vitu vinavyopelekea vidonda (vitu vye ncha kali) husababisha vidonda ambapo vimelea vinaweza kukaa. Pia mnyama anaweza kupata ugonjwa kutokana na hali za ndani ya mwili k**a upungufu wa lishe, mfano: madini na magonjwa ya mfano wa wadudu hao ni;
VIMELEA (BAKTERIA)
☆Mfano wa magonjwa yanayosababishwa na bakteria ni chambavu, blackquartet, kimeta, kifua kikuu, brucellosis (ugonjwa wa kutupa mimba) na ugonjwa wa kiwele. Ng'ombe dume huvimba mapumbu
VIRUSI OTASIS
☆Mfano wa magonjwa yanayosababishwa na virusi ni kichaa cha mbwa (rabies). Ugonjwa wa midomo, miguu (foot and mouth dsease) na sotoka (rinderpest)
PROTOZOA
☆Magonjwa yanayo sababishwa na protozoa ni k**a ndigana baridi, ndigana kali, ndigana mkojo damu, ndigana maji moyo na nagana.
ANGALIZO
☆Magonjwa yote ya Ndigana husambazwa na makupe, wakati ugonjwa wa nagana husambazwa na ndorobo
LISHE DUNI
☆Upungufu wa viinilishe katika chakula cha mifugo husababisha madhara katika mwili k**a ifuatavyo;
☆Husababisha majike kutopata joto mapema
☆Ndama kuzaliwa na viungo visivyo komaa
☆Upungufu wa uzalishaji maziwa
☆Kiwango cha uzalishaji kushuka
VIDONDA/MICHUBUKO
☆Kupitia vidonda au michubuko, wadudu wasababishao magonjwa huweza kuingia mwilini kwa mnyama.
MAGONJWA YA KURITHI
☆K**a mmoja wa wazazi ana ugonjwa wa kurithi basi kuna uwezekano mkubwa kwa mmoja wa ndama watakaozaliwa kurithi ugonjwa huo
MAGONJWA YANAYOENEZWA NA KUPE
NDIGANA KALI
Dalili zake
☆Homa kali hadi nyuzi joto 42C
☆Povu kutoka mdomoni na puani
☆Kuhara choo kilichochanganyika na k**asi na damu
☆Tezi kuvimba sana na zenye joto
☆Kuacha kula
☆Ukungu kwenye macho
☆Kifo baada ya wiki moja hadi mbili
TIBA
☆Butalex, Parvexon, tiba iambatane na sindano moja ya kuondoa uvimbe kwenye mapafu k**a hali hiyo tayari imeshajitokeza. Tumia multivitamin ili kuongeza hamu ya kula na Raxis ili kuondoa maji kwenye mapafu.
KINGA/ZUIA
☆Zingatia uogeshaji sahihi na chanjo ya ECF
NDIGANA BARIDI (Anaplasmosis)
Dalili zake
☆Homa hadi nyuzi joto 42C
☆Kukosa hamu ya chakula
☆Choo kigumu na mak**asi ya harufu mbaya
☆Kifo baada ya siku 8 hadi 10
TIBA
☆Antibiotic k**a vile Oxytetracycline
☆Imizol
KINGA
☆Zingatia uogeshaji sahihi
NDIGANA MKOJO DAMU (BABESIOSIS) UGONJWA WA KUKOJOA DAMU
Dalili zake
☆Mkojo kuwa na rangi ya damu isiyokolea zambarau
☆Mkojo kutoka kidogo kidogo na kwa muda mrefu
☆Homa hadi nyuzi joto 40C
☆Kuacha kula
☆Choo kigumu au kuhara wakati mwingine
☆Kifo baada ya wiki moja
TIBA
☆Berenilikisaidiwa na antibiotics za sindano k**a vile oxytetracycline (OTC) pia tumia multivitamin kuongeza hamu ya kula
KINGA
☆Zingatia uogeshaji sahihi
NDIGANA MAJI MOYO (HEART WATER)
Dalili zake
☆Kizunguzungu na kuanguka
☆Kifo baada ya siku mbili
TIBA
☆Antibiotics za sindano k**a vile oxytetracycline. Kumbuka tiba lazima ifanywe mapema iwezekanavyo
KINGA/KUZUIA
☆Zingatia uogeshaji sahihi
UTUNZAJI WA KUMBUKUMBU
☆Uwekaji wa kumbukumbu ni muhimu sana kila kila mfugaji. Kumbukumbu zinasaidia katika kujua mambo mengi k**a matukio ya magonjwa, tiba, chanjo na uogeshaji, mishahara ya wafanyakazi, faida au hasara baada ya mauzo. Kumbukumbu hizi humsaidia mfugaji kufanya maamuzi katika uendelezaji wa shamba lake.
AINA ZA KUMBUKUMBU
☆Kumbukumbu muhimu katika ufugaji wa ng'ombe ni pamoja na idadi ya ndama wanaozaliwa, idadi ya ng'ombe, afya ya ng'ombe, kumbukumbu ya mapato na matumizi.
Hata hivyo mfugaji anaweza kuongeza kumbukumbu nyingine kulingana na mahitaji na shughuli zake..
Kwa Maelezo Zaidi au Ushauri Tuwasiliane Kupitia
Martin Ahadiel Animal Health Care Whatsap No
0657338499..

FAHAMU AINA ZA KUKU NA FAIDA ZAKE.Kuna aina mbalimbali za kuku ambazo mfugaji anaweza kufuga na kila aina inategemeana n...
29/01/2019

FAHAMU AINA ZA KUKU NA FAIDA ZAKE.
Kuna aina mbalimbali za kuku ambazo mfugaji anaweza kufuga na kila aina inategemeana na malengo ya mtu husika anayetaka kufanya shughuli hii ya ufugaji, hivyo leo nimekuletea makundi makuu manne ya kuku ambayo tunayafuga hapa Tanzania.
KUKU WA NYAMA.
Hii ni moja ya kundi la kuku ambalo linafugwa sana hapa nchini na kuku hawa wanafugwa kwa malengo ya kuzalisha nyama tu. Uzalishaji wa kuku hawa wanachukuliwa kuku wazazi kutoka nje ya nchi na kuhifadhiwa sehemu maalumu kwa ajiri ya kuzalisha mayai na mayai yanatotoreshwa na kupata vifaranga kwa ajili ya nyama ,
Faida ya kuku hawa.
Faida ambayo utaipata k**a mfugaji ni kuwa kuku hawa hufugwa kwa mda mchache muda wa miezi miwili au mitatu na kuuzwa kwa ajili ya matumizi ya nyama, hivyo ni sehemu nzuri yakujipatia kipato na kunufaika na ufugaji wako kwa muda mfupi.
Zingatia.
Gharama za kuwalea kuku hawa ni kubwa kidogo hivyo unapoamua kufanya ufugaji kwa ajili yakupata tija katika kukuza kipato chako ni muhimu ukafuga kuku wengi kwa wakati mmoja hii itakufanya upate faida nzuri kuliko kufuga kuku wachache na ukapata hasara na kuona ufugaji haulipi kumbe wewe mwenyewe haukuwa na taarifa kamili kuhusu ufugaji wako.
Muhimu.
Ni muhimu sana kutunza kumbukumbu za gharama za matumizi katika mradi wako wa kuku ili pale utakapo uza uweze kujifanyia tathmini na kujua umepata faida au hasara katika mradi wako.
KUKU WA MAYAI.
Hawa ni aina ya kuku ambao hufugwa kwa malengo maalumu ili kuzalisha mayai, kuku hawa wanataga kwa wingi sana mayai na wanataga bila jogoo, kuku hawa wamendaliwa vizuri kwa ajili ya kutaga tu hivyo k**a utaamua kuwawekea jogoo watataga na kuatamia lakini vifaranga wake watakuwa hawana ubora ule unaotakiwa.
Faida ya kuku hawa.
Kwakuwa kuku hawa ni watagaji wazuri wa mayai basi wanampatia mfugaji uhakika wa kipato kwa kila siku hadi pale atakapofikia mwisho wa mradi wake, yaani miaka miwili.
Zingatia.
Ili kupata faida iliyokusudiwa katika mradi wako huu wa kuku unatakiwa uwape chakula bora na cha kutosha pia uzingatie chanjo na tiba kwa magonjwa pale unapoona dalili ya magojwa.
Muhimu.
Ufugaji wakuku ni moja ya aina ya miradi yenye faida nzuri iwapo tu mfugaji atazingatia kanuni bora za ufugaji. Ufugaji huu ili ukuletee tija ni muhimu ukafuga kuku wengi angalau mia tatu na kuendelea hapo utaiona faida yake nzuri.
KUKU CHOTARA.
Hawa ni aina ya kuku ambao wamechanganya aina fulani ya kuku na aina nyingine ya kuku na kupata aina moja ya kuku, mfano: amechukuliwa jogoo wa kienyeji akachanganywa na tetea wa kisasa na vifaranga vitakavyotoka vitakuwa chotara kwa maana watakuwa na sifa baadhi za kienyeji na sifa baadhi za kisasa.
Kuku hawa kwa hapa nchini wapo wengi na kuna makundi mbalimbali ya kuku kulingana na asili na mahali walipo tokea, mfano: MALAWI, KENBRO, SASO na KROILA na hawa wanatofautiana sifa na asili.
Faida ya kuku chotara.
Hapa nitataja kwa ujumla faida zote ila wakati mwingine nitachambua aina moja moja ya kuku chotara.
Wanakuwa kwa haraka na wanakuwa na maumbo makubwa tofauti na kuku wakienyeji hivyo ni wazuri sana kwa nyama.
Ni watagaji wazuri sana tofauti na kuku wakienyeji (kuku hawa ukuwahudumia vizuri wanataga mayai kati ya 180-300 kwa mwaka hivyo ni wazuri sana kwa mayai.
Wanaishi kwenye mazingira yeyote yale kwa maana wanaweza kuishi vizuri wakiachiwa kujitafutia chakula.
Wanastahimili sana magonjwa (chanjo ni Muhimu kuwapa) tofauti na kuku wa nyama au wa mayai.
Nyama yao ni nzuri sana haina tofauti na kuku wakienyeji.
Wanauzito mkubwa kuku mmoja anafika hadi kilo sita.
Soko lake ni kubwa.
KUKU WAKIENYEJI.
Hawa ni kuku ambao asili yake ni hapa hapa Tanzania na tunao katika maeneo mengi ya nchi yetu, kuku hawa wanakuwa wana maumbo madogo kulinganisha na kuku chotara, pia kuku hawa hawakui kwa haraka ukilinganisha na kuku chotara, aina hii ya kuku hutaga mayai machache sana kwa mwaka na wanataga mayai kati ya 40-120.
Faida ya kuku hawa.
Kuku hawa wanafugika katika mazingira yeyote yale kwa sababu ni wazuri kujitafutia chakula, ili upate faida nzuri ya mradi wako wa kuku huo unashauriwa kuwapa chakula cha ziada ili waweze kukua kwa haraka na kuwa na uzito mzuri.
Kuku hawa hawana gharama hivyo nashauri k**a una eneo zuri ni muhimu ukaanza ufugaji wa kuku hawa kwa sababu hawana shida katika ufugaji wake.
Kuku hawa wanapendwa sana hapa nchini kwa sababu ya nyama na mayai yake kuwa mazuri sana na ni kuku wa asili hivyo tunaamini hawana kemikali na hii ni kweli kabisa,
Hizi ni aina mbalimbali za kuku katika nchi yetu na jambo la muhimu kuangalia malengo yako na uhitaji ya jamii husika jambo nzuri na lakuvutia ni kwamba aina hizi za kuku zinafugika katika maeneo yetu yote ya nchini hivyo angalia mazingira yako na anza kufanya ufugaji.

LISHE YA KUKU:Ili kuku waweze kuishi, kukua vizuri, kunenepa na kutaga mayai mengi ni lazima wale chakula kingi na cheny...
18/01/2019

LISHE YA KUKU:
Ili kuku waweze kuishi, kukua vizuri, kunenepa na kutaga mayai mengi ni lazima wale chakula kingi na chenye ubora unaotakiwa. Uwingi na ubora wa
lishe ya kuku unaweza kuainishwa katika makundi ya vyakula k**a ifuatavyo:
1. Vyakula vya kutia nguvu
2. Vyakula vya kujenga mwili
3. Vyakula vya kuimarisha mifupa
4. Vyakula vya kulinda mwili
5. Maji.

1. Vyakula vya kutia nguvu:
Vyakula vya mifugo vifuatavyo vinawekwa katika kundi hili;
a. Pumba za mahindi, pumba laini za mpunga, na, pumba laini za ngano.
b. Nafaka k**a vile mtama , chenga za mahindi ,chenga za mchele, uwele , na ulezi
c. Mimea ya mizizi k**a vile muhogo, viazi vitamu na magimbi. Kabla ya kulisha kuku hakikisha mizizi hiyo inalowekwa kwa muda wa saa moja au kupikwa kabla ya kukausha ili kuondoa sumu ambayo kwa asili imo katika vyakula vya aina hii.Inashauriwa kuwa mizizi hiyo ilishwe kwa kiasi cha asilimia 10% ya chakula chote anacholishwa kuku.
Katika kundi hili la kutia nguvu ,vyakula vya mafuta k**a vile mafuta ya kutoka kwenye vyakula vya mafuta k**a mashudu ya mimea ya mafuta, mafuta ya samaki husaidia kuongeza nguvu na joto mwilini. Vyakula vya kutia nishati huchangia asilimia 60-70 ya mchanganyiko wote wa chakula.

2. Vyakula vya kujenga mwili:
Ø Mashudu :Haya ni makapi ya mbegu za mimea aina ya mikunde na vyakula v vinavyotoa mafuta k**a vile alizeti, mawese, karanga, soya ,korosho, na ufuta .
Ø Damu ya wanyama iliyokaushwa (waliochinjwa na kukaguliwa), hii inafanywa ili kuepusha uwezekano wa kuku kupata magonjwa ya kuambukiza .
Ø Mabaki ya samaki ya samaki/dagaa na nyama.
Ø Vyakula asilia k**a vile minyoo, mayai ya mchwa, Masalia ya nyama toka kwenye ngozi/mifupa, wadudu walioteshwa kutokana na damu au nyama iliyooza na vyakula vya aina nyingine.
Ø Vyakula hivi huchangia asilimia 20 hadi 30% ya mchanganyiko wote wa chakula cha kuku.

3. Vyakula vya kuimarisha mifupa(madini):
a)Hivi ni vyakula vya madini ambavyo huhitajika kwa ajili ya kujenga mifupa, maganda ya mayai, kukua na kuuweka mwili wa ndege (kuku) katika hali ya afya njema kwa ujumla.
b) Madini ya muhimu ni madini ya chokaa (calcium) na fosiforasi (phosphorus). Ili kuku watage mayai yenye ganda gumu ni lazima wapate madini ya chokaa maganda ya konokono na mayai yaliyosagwa vizuri. Lakini inapendekezwa kwamba unapoongeza madini ya fosforasi inakubidi uongeze pia madini ya chokaa kadri inavyopasa ,kwasababu kiwango cha aina moja kikizidi kuliko cha aina nyingine husababisha upungufu wa kile kidogo
Viinilishe vya madini vinavyotakiwa ni pamoja na;
Ø Majivu ya mifupa yaliyosagwa vizuri, unga uliosagwa wa magamba ya konokono wa baharini, konokono wa nchi kavu na maganda ya mayai yaliyochomwa . Kabla maganda ya mayai na nyumba za konokono havijatumika inashauriwa yachomwe moto mkali au yachemshwe ili kuua vijidudu vya maradhi.
Ø Chumvi ya jikoni
Ø Madini yaliyotengenezwa viwandani k**a vile Di-calcium phosphate
Ø Magadi (kilambo).

4.Vyakula vya kulinda mwili:
Hili linajumuisha vyakula vya mbogamboga k**a vile;
Ø Mchicha, samadi ya ng’ombe ambayo haijakaa muda mrefu baada ya kunyewa, mchicha pori, Chinese kabeji n.k.
Ø na Mchanganyiko wa vitamini uliotengenezwa na viwanda vya madawa (vitamin premix).
Ø Jua ni muhimu katika kuhakikisha vitamini A na D zinatumika vizuri mwilini, kwahiyo banda ni lazima lijengwe kwa mtindo ambao unaruhusu mwanga kupita hasa nyakati za asubuhi na jioni.
Ø Chakula cha kuku wanaofugwa ndani ni lazima kichanganywe na vitamini zinazotayarishwa viwandani.

FAHAMU UGONJWA WA MAFUA YA KUKU..Mafua ya kuku husababishwa na virusi ambao wapo wa aina tofauti kwa kuku, bata na ndege...
15/01/2019

FAHAMU UGONJWA WA MAFUA YA KUKU..
Mafua ya kuku husababishwa na virusi ambao wapo wa aina tofauti kwa kuku, bata na ndege. Ugonjwa huu hujulikana k**a mafua ya ndege au avian influeza kwa kingereza kwani kuna aina ya virusi ambavyo husababisha ugonjwa huu kwa ndege wa porini, kwa kuku ugonjwa huu huwapata kuku wa kubwa na wadogo.

Dalili za mafua ya kuku.
Dalili za mafua ya kuku huanza kuonekana kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba. Dalili hutofautiana na umri wa kuku, aina ya kuku,na ukubwa wa kuku maranyingi kuku wa wiki moja hadi wiki nane wana vimba kichwa na sehemu za usoni huwa na uvimbe baadae kope za macho hugandamana pamoja na kutiririka mak**asi japo kutiririka mak**asi kunatokea kwa kuku wakubwa pia ugonjwa huu husababisha vifo kwa kuku wadogo ambao huathiriwa kwa kutoona na kushindwa kufikia chakula na maji maranyingi kuku wana dhohofika, wanapiga chafya,kutokwa na mak**asi na machozi. Kuku ambao wanataga hupunguza utagaji kwa asilimia 90% na wakitaga mayai yanakuwa malaini. Pia kuku husinyaa na hushusha mabawa, kuku walio athirika na ugonjwa huu watasinyaa atak**a hawatakufa.

Matibabu na jinsi ya kuzuia
Tumia dawa aina zifuatazo kwa kufuata muongozo wa kwenye karatasi au kwenye kifungishio.
ANTIBIOTIC,SULPHEAMETHAZINE, OFULIDONE, FLUMEQUINE, FERAMYCINE na STREPTOMYCINE.
Ugonjwa huu huzuiliwa kwa kutoa chanjo kwa kuku wadogo na wakubwa, pia kuku wagonjwa wanatakiwa kutengwa na kuku wazima, safisha nyumba na vyombo kwa dawa (disinfectant) kabla ya kuweka vifaranga au kuku wapya pia tumia matandiko yasiyo na vumbi.

31/12/2018

Vipimo vya kawaida vinatumika shambani/bandani kupima dawa ama Chakula
Bandani ni vigumu kuwa na mizani hasa kupima dawa ama Chakula japo ni muhimu kuwepo. Hebu tuangalie vipimo mbalimbai vinavyotumika bandani kwa kuku
1: Kijiko kidogo cha chai
Ujazo wa Kijiko hiki huwa ni sawa na gramu 5 za dawa ya unga ama chengachenga.
2. kijiko kikubwa cha chai/Chakula
Ujazo wa Kijiko hiki ni sawa na gramu 10 za sawa za Unga au chengachenga
3: Ganda au kasha la kiberiti
Ujazo Wa kasha hiki huwa sawa na gramu 10 za sawa ya Unga ama chengachenga
Upimaji Wa Chakula
Upimaji Wa Chakula una trick kidogo. Maana uzito Wa Chakula hutegemea raw materials zilizotumika Kutengeneza Chakula hicho
kwa uzoefu kwa Chakula kilichochanganywa virutubisho vyote kitaalamu:,
1: ujazo wa Ndoo ya Lita 10 unakuwa sawa na kilo 7-8 za Chakula
2: Ujazo Wa ndoo ya Lita 20 unakuwa sawa na kilo 14-15
3: ujazo Wa sadolin kubwa unakuwa sawa na kilo 2.5-3 za chakula
Jaribu kufanya utafiti Wa Chakula mwenyewe utaona. Inaweza kuwa tofauti kulingana na aina ya Chakula chako
kwa kawaida kuku mkubwa hula gramu 100-130 ambazo ni sawa na ujazo Wa kiganja cha mkono Wa MTU mzima yaani konzi moja.....
Kwa maelezo zaidi au ushauri tuwasiliane kupitia
MartinAhadiel Animal Health Care
0657338499..

 :KIDERI/MDONDO(Newcastle disease).Ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege ambao unasababishwa na vimelea aina yaparamyxovi...
24/12/2018

:
KIDERI/MDONDO(Newcastle disease).

Ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege ambao unasababishwa na vimelea aina ya
paramyxovirus.

:

Ugonjwa wa Mdondo (Newcastle disease) huenea kupitia njia mbalimbali k**a zifuatazo:-
Mayai ya kuku aliyeugua ugonjwa wa mdondo/kideri (Newcastle disease).
Kugusana na kuku mgonjwa.
Kupitia maji yenye maambukizi.
Wakati wa totoleshaji vifaranga.
Chakula chenye maambukizi.
Hewa yenye maambukizi ya ugonjwa huu.

(Newcastle disease);

1. Vifo vya ghafla.
2. Kutoa udenda mdomoni.
3. Kukosa hamu ya kula.
4. Kuharisha kinyesi cheupe na kijani.
5. Kuhema kwa shida.
6. Kukak**aa viungo au kupooza hasa mabawa, shingo na miguu.
7. Kupunguza utagaji.
8. Vifo hutegemea kasi ya ugonjwa huweza kufikia hadi asilimia mia moja (100%).

/Kideri (Newcastle disease);

1. Wapewe chanjo kwa muda unaofaa (Siku ya 7 na 28, na kila baada ya miezi 3).
2. Kuku wote waliozidiwa (wagonjwa) wachinjwe na wafukiwe katika shimo lenye kina kirefu kuzuia kuenea ugonjwa.
3. Fuata maelekezo ya Daktari au Mtaalam wa mifugo.



*Hakuna matibabu ya ugonjwa huu, ila KUKU wanaweza kupatiwa antibiotic kwajili ya maambukizi nyemelezi. kwa msaada na ushauri zaidi katika ufugaji wasiliana na Daktari au tupigie simu nambari; 0657338499..

UFUGAJI WA MBUZI; SEHEMU YA 5UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO WA MIEZI4-8:-Ili kondoo/mbuzi aweze kukua na kupevuka mapema zinga...
15/12/2018

UFUGAJI WA MBUZI; SEHEMU YA 5
UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO WA MIEZI4-8:-Ili kondoo/mbuzi aweze kukua na kupevuka mapema zingatia mambo yafuatayo:-
Kumpatia chakula cha ziada kwa miezi 2 mfululizo kiasi cha kilo0.2-0.7 kwa siku kuanzia anapo achishwa kunyonyesha.
Kumpatia dawa za kuzuia minyoo k**a iatakavyo shauriwa na mtaalam wa mifugo na aogeshwe mara kwa mara ili kuzuia magonjwa.
Kukata kwato zikikomaa.
UMRI WA KUPANDISHA:-Wakitunzwa vizuri wanaweza kupandishwa wakiwa na umri wa miezi 8-12 kwa walioboreshwa miezi18-24 kwa mbuzi wa asili iatategemea na afya alonayo pia inashauriwa apandishwe akiwa na uzito wa kilo 12.
DALILI ZA JOTO:-
Hutingisha mkia
Hutoa ute mweupe ukeni
Hufuata dume
Hamu ya kula hupungua
Hukojoa mara kwa mara
Uke huvimba na huwa mwekundu kukiko kawaida
Huangaika mara kwa mara na kupiga kelele
Kwa mbuzi anayekamuliwa hupunguza kiwango cha maziwa.
Mbuzi/kondoo mwenye dalili hizi apelekwe kwa dume na uchunguze tena dalili za joto baada ya siku 19-21
Msimu mzuri wa kuzaa ni baada ya mvua.
UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO MWENYE MIMBA:-
Mbuzi hubeba mimba kwa muda wa miezi 5
Apewe chakula cha ziada 0.2-0.7.
Apewe nyasi,miti malishi na mikunde mchanganyiko kilo 1.8-2.5 kwa siku
DALILI ZA KUKARIBIA KUZAA:-
Huangaika kwa kulala na kuamka mara kwa mara
Hujitenga na kundi na hufuata sehemu kavu na yenye kivuli
Hutokwa na ute mzito ukeni
Hupiga kelele
Pindi ukiona dalili hizi muandalie sehemu maalum ya kuzalia na muwekee maji ya kutosha.
UTUNZAJI WA MBUZI/KONDOO ANAYE NYONYESHA:-
Huhitaji chakula zaidi kwa kuzalisha maziwa na chakula ya kitoto pamoja na nyasi,mikunde na majani ya miti malisho kilo 1.8-2.5 kwa siku ni muhimu apewe nyongeza ya 0.3-0.8 kwa kila lita inayoongezeka na maji safi na slama wakati wote
UKAMUAJI WA MAZIWA:-Sehemu ya kukamulia safi na tulivu.
Awe na afya nzuri,msafi kiwele kioshwe na maji safi ya uvuguvugu.
Mkamuaji asibadilishwe badilishwe,awe msafi mwenye kucha fupi na asiwe na magonjwa ya kuambukiza.
Vyombo vya kukamulia view safi.
Maziwa ya mwanzo yakamuliwe kwenye chombo malum(strip cup)kwa uchunguzi wa ugonjwa wa kiwele.
UTUNZAJI WA DUME BORA LA MBEGU:-
Dume la mbegu linahitaji matunzo mazuri ili litoe mbegu bora kupanda na kuzalisha.
Dume bora huanza kupanda akiwa na miezi 8-10 msimu wa kupandisha dume 1 lipandishwe majike 40-50 inashuriwa madume yenye miezi 8-9 yapandishwe majike ambayo ni mara ya kwanza kupandwa.
Malisho ya kutosha na chakula cha ziada kisipungue kilo 0.2-0.7 kila siku na maji ya kutosha.
Majani ya miti yenye lishe,mikunde na nyasi na mabaki ya mazao pia kilo 0.45-0.9 za chakula cha ziada kulingana na uzito wake na wingi wa majike anayopanda wiki 2 kabla.....

Address

Morogoro

Telephone

+255657338499

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Martin Ahadiel Animal Health Care posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Martin Ahadiel Animal Health Care:

Share

Category