20/04/2026
KWA NINI NG'OMBE ANAKATA MAZIWA WAKATI WA STRESS?
STRESS HUPANDISHA ADRENALINE NA KUSHUSHA OXYTOCIN HOMONI
Homoni ya adrenaline( homoni ya "mapambano) ina athari ya haraka katika kuzuia maziwa yasitoke. Hii hutokea pale ng'ombe anapopata -hofu,
- maumivu, au
-msongo wa mawazo.
Inafanyaje kazi dhidi ya uzalishaji na utoaji wa maziwa?
1. Kuzuia Homoni ya Oxytocin
Ili maziwa yashuke mwili wa ng'ombe unahitaji homoni (oxytocin).
- Adrenaline inafanya kazi kinyume kabisa na oxytocin. Ng'ombe anapopata mshtuko au hofu, adrenaline huzuia ubongo kutoa oxytocin kwenye mzunguko wa damu. Bila oxytocin, misuli midogo inayozunguka mifuko ya kuhifadhi maziwa (alveoli) haitajikunja, hivyo maziwa hayashuki kuelekea kwenye chuchu.
2. Kusinyaa kwa Mishipa ya Damu (Vasoconstriction)
Adrenaline husababisha mishipa ya damu kusinyaa ili kupeleka damu nyingi kwenye misuli na moyo. Hii inapunguza kiasi cha damu kinachofika kwenye kiwele. Kwa kuwa oxytocin husafiri kupitia damu ili kufika kwenye kiwele, mishipa ikisinyaa, oxytocin ndogo iliyobaki inashindwa kufika kwenye seli zinazohusika na utoaji wa maziwa.
3. Matokeo ya Muda Mfupi na Mrefu
Muda mfupi: Wakati wa ukamuaji, utaona ng'ombe "amebana" maziwa. Unaweza kupata maziwa kidogo sana au usipate kabisa, hata k**a kiwele kinaonekana kimejaa.
Muda mrefu: Maziwa yakibaki kwenye kiwele kwa sababu ya adrenaline, shinikizo ndani ya kiwele huongezeka. Hii inatuma ishara mwilini kuwa hakuna haja ya kutengeneza maziwa mengine mapya, hivyo kiwango cha uzalishaji huanza kushuka rasmi siku hadi siku.
Vitu vinavyochochea Adrenaline (Zingatia Kuepuka Hivi):
-Kupiga au kupigia kelele ng'ombe wakati wa ukamuaji.
-Mbwa kubweka au wanyama wengine kusumbua karibu na banda.
-Kubadilisha mfanyakazi (mkamuaji) ghafla au kubadilisha ratiba ya kawaida.
-Vifaa vya kukamulia vyenye hitilafu vinavyosababisha maumivu au mshtuko wa umeme.
Kidokezo: Ili kuepuka adrenaline, mkamuaji anapaswa kumfanyia ng'ombe masaji ya kiwele kwa maji ya uvuguvugu na kuhakikisha mazingira ni tulivu. Hii inashusha adrenaline na kupandisha oxytocin, jambo linalofanya maziwa yatoke kwa urahisi na kwa wingi zaidi.
"TUISHI HUMU"