14/05/2019
UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA PEREGE/SATO WANAOKUZWA UTOMWILI(PROTEIN) 28%
Dagaa 18.25g
Unga wa soya 25g
Pumba za mpunga 6g
Unga wa muhogo 36.42g
Unga wa alizeti (mashudu) 10g
Vitamin-mineral mix 4.33g
UTENGENEZAJI WA CHAKULA CHA SAMAKI WAZAZI PEREGE(SATO) 44%
Dagaa 36.2g
Corn gluten meal 20.4g
Unga wa soya 17.7g
Copra meal 11.8g
Starch 3.2g
Cod liver oil 3.2g
Mafuta(vegetable oil) 0.5g
Vitamin-mineral mix 0.5g
Pumba za mchele 7.5g
Zingatia;
Lisha samaki wako katika eneo maalum na kwa wakati ule ule kilasiku. Hii itasaidia samaki wako kula chakula chote kwa sababu muda wa kula ukifika watakuwa katika eneo walilozoeshwa. Pia unaweza kuwafundisha samaki wako kula kwa mwitikio, yaani kabla ya kulisha gonga kengele au kitu chochote kinachoweza kutoa mlio kisha walishe. Fanya zoezi hili kila unapotaka kuwalisha hivyo watazoea.
Wakati unalisha anza kwa kiasi kidogo cha chakula na samaki wanapojaa katika eneo husika endelea kuongeza chakula hadi kiasi ulichopima kitakapoisha. Hakikisha ukubwa wa punje za chakula zinaendana na ukubwa / umri wa samaki. Kwa kawaida samaki wadogo hulishwa chakula cha unga na wakubwa hulishwa chakula cha punje(pellets).